Watu Zaidi ya 37 Wafariki Dunia Katika Mapigano ya Wakristo na Waislamu

Watu Zaidi ya 37 Wafariki Dunia Katika Mapigano ya Wakristo na Waislamu
WATU zaidi ya  37 wamekutwa wamefariki katika mji mmoja katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kutokana na mapigano kati yaWakristo na Waislam ambapo kanisa moja lilichomwa moto.

Katika taarifa ya Umoja wa Mataifa ya jana (Ijumaa) mapigano hayo ambayo yanajumuisha zaidi wanamgambo, padri mmoja aliuawa Alhamisi katika mji wa  Alindao wakati wanamgambo wa Kikristo walipoua Waislam kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya Waislam.

Umoja huo umethibitisha vifo vya watu 37 waliokutwa katika mji wa Alindao, ambapo watu 20,000 wameyakimbia makazi yao.

Ikiwa moja ya nchi maskini zaidi duniani, licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa almasi na uranium, nchi hiyo imekumbwa na vita vya ndani tangu mwaka 2013 wakati Rais Francois Bozize ambaye ni Mkristo, alipinduliwa na waasi wa kundi la Seleka ambao wengi ni Waislam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad