Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga, Zainabu Abdallah amebainishwa kuwa yeye ndiye mkuu wa wilaya ya mdogo kuliko wote nchini na kuonngeza kuwa alikumbana na changamoto nyingi wakati anaanza majukumu yake baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli.
Akizungumza katika kipindi cha East Afrika Breakfast Zainabu amesema wakati akiwasili ofisini kwa mara ya kwanza aliwahi kudharaulika na baadhi ya watumishi wake kutokana na umri wake hali ambayo ilimfanya kumrudisha nyuma kidogo kwenye majukumu yake ya uongozi.
“Ni kweli mimi ndiye Mkuu wa Wilaya mdogo mpaka sasa nina miaka 25 tu lakini wakati nateuliwa baadhi ya watumishi wangu wilayani walikuwa wananidharau sababu umri wangu ulikuwa mdogo na walidhani nilikuwa nimebebwa kupata uongozi bila kujua historia yangu ya uongozi.” Zainabu Abdallah
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema wilaya yake inaongoza kwenye uzalishaji wa zao la nazi hivo amewataka wawekezaji nchni kuangalia namna ambavyo watavutiwa kuwekeza kwenye wilaya ili kuhimiza Tanzania ya viwanda.
“Tuliwapelekea sampo ya mbolea inayotokana na nazi wawekezaji wa Kilimanjaro walisifia sana, lakini sio nazi tu tuna mazao mengine kama muhogo, kwa hiyo ukiwekeza kwenye mihogo, unaweza ikakufaidisha kimaisha, lakini pia tumeweka kipaumbele kwenye zao la korosho wakija watapata maeneo ya kuwekeza. ” amesema.
Wilaya ya Pangani inachangia zaidi ya asilimia 70 ya zao la mkonge nchini, ambapo pamoja na mabo mengine mkuu huyo wa wilaya amewataka watu kutumia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta ambao linajengwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Uganda.