Imeelezwa kuwa ni kosa kwa muuzaji wa duka la dawa kutoa dawa kwa mgonjwa bila cheti kutoka kwa daktari, na endapo mfamasia akigunduliwa kuwa anatoa dawa kiholela anaweza kufungiwa biashara na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Akizungumza kwenye East Africa BreakFast ya East Africa Radio, Mfamasia kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Mary Masanja amesema kuwa imekuwa ni tabia ya wengi kunywa dawa kwa mazoea ni kosa kwa mujibu wa sheria na muuzaji anaweza kuchukuliwa sheria.
Mary amesema kuwa duka lolote la dawa linatakiwa kuwa na mtaalam wa madawa na mwenye elimu ya afya ili kutoa ushauri pia namna ya matumizi sahihi ya dawa.
"Hakuna Antibiotic inayotibu Malaria kama wengi wanavyodhani kuwa dawa hiyo ina msaada kwenye kila ugonjwa, na kuna wakati dawa hizi zikitumika ovyo husababisha kuua baadhi ya bakteria wanaolinda kinga mwili", amesema Mary.
Mary ameongeza kuwa, "Ni kosa kwa muuzaji wa duka la dawa kutoa dawa kwa mgonjwa bila cheti kutoka kwa daktari, imekuwa ni tabia ya wengi kunywa dawa kwa mazoea ni kosa kwa mujibu wa sheria na muuzaji anaweza kuchukuliwa sheria na kufikishwa mahakamani".
Hayo yanajiri ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya matumizi ya dawa za 'Antibiotiki' ambapo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto inatoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ili kuepusha ongezeko la magonjwa yanayosababishwa na matumizi mabaya ya dawa.
Wauza Dawa Wapigwa Stop Kuwauzia Dawa Wagonjwa Bila Cheti cha Daktari
0
November 14, 2018
Tags