Wawili “Wasukumwa ndani”, Korosho za Magufuli
0
November 20, 2018
Hamisi Musa ambae ni karani wa Chama cha msingi cha Ushirika cha Mayanga tawi la Likonde Mkoani Mtwara pamoja na kijana Shafii Namahala wamejikuta wakiishia mikononi mwa polisi baada ya kuhamishia mizani ya kupimia korosho pamoja na shughuli zote za chama nyumbani kwao.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amefika nyumbani kwa mkulima Shafii Namahala na kukuta shughuli za upimaji zikiendelea , huku tayari magunia 134 yamekwisha andaliwa kwa ajili ya kusafirishwa.
Akizungumza nyumbani kwa Mkulima huyo, Dc Mmanda amesema kilichofanyika ni ukiukwaji wa maagizo na taratibu zilizowekwa kwani sheria inamtaka mkulima kubeba Korosho zake kutoka Nyumbani kwa kutumia vifungashio vyake hadi Ofisi ya Chama cha Msingi cha Ushirika ambapo ndipo zoezi la uhakiki wa ubora linafanyika,
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amempokea Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dr. Hussein Mwinyi katika uwanja wa Ngede wa Mkoani Mtwara ambaye aliambatana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la hilo Luteni Jenerali Yakubu Mohamedi.
Tags