Waziri Lugola Awaambia Mabalozi Nchi Ipo Salama.....Aahidi Kuendelea Kushirikiana Nao

Waziri Lugola Awaambia Mabalozi Nchi Ipo Salama.....Aahidi Kuendelea Kushirikiana Nao
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia, Kenya na Afrika Kusini katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, na kuwaambia ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao nchini upo vizuri.

Akizungumza katika kikao cha mabalozi hao waliofika ofisini kwake kwa nyakati tofauti leo, Lugola pia aliwaomba wawakilishi hao wa nchi zao hapa nchini waendelee kushirikiana na Wizara yake na nchi kwa ujumla.

Lugola aliwahakikishia Mabalozi hao kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.

“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Balozi wa Afrika Kusini, Thami Mseleku alisema akiwa nchini anajiona kuwa yupo nyumbani kwasababu nchi yake ina historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania.

Hata hivyo, Balozi wa Italia, Roberto Mengoni alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya nchi yake na Tanzania.

“Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Mengoni.

Naye Balozi wa Kenya Nchini, Dan Kazungu alisema Tanzania ni nchi yake na anajisikia furaha kuwepo nchini kwasababu alishawahi kufanyakazi miaka kadhaa iliyopita hapa nchini, hivyo nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad