Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa, anatarajiwa kutembelea Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Jumamosi ya tarehe 17, November 2018 .
Taarifa iliyotolewa hii leo Novemba 15, na Mbunge wa Nachingwea, Mhe. Hassani Masala inasema kuwa, Mhe. Waziri mkuu atatua uwanja wa ndege wilayani Nachingwea mnamo saa mbili asubuhi akitokea Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Rukia Muwango pamoja na viongozi wengine wa serikali, kisha Waziri atafanya ziara ya siku moja katika wilaya hiyo kwa kutembelea tarafa ya kilimarondo.
"Mhe. Waziri Mkuu akiwa njiani kuelekea kilimarondo atasalimia wananchi wa Mtua na Mbondo kisha Mkutano wa hadhara mkubwa utakaobeba ujumbe wa wilaya utafanyika Kilimarondo na kujumuisha wananchi wote wa Kilimarondo,Matekwe na kiegei, lakini Pamoja na kusalimia Wananchi na kusikiliza kero zao, Mh Waziri Mkuu atakagua na kujionea Ujenzi wa kituo cha Afya Kilimarondo" Amesema Mhe. Masala.
Mbunge Masala amewaasa Wananchi wa Nachingwea tujitokeza kwa wingi saa moja asubuhi uwanja wa ndege tayari kwa kupokea ugeni huu aliosisitiza kuwa ni ugeni wa heshima kwao kama wilaya.
Nachingwea ni wilaya inayoongoza kwa kuzalisha Korosho nyingi mkoani Lindi kwa Msimu uliopita na hata huu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kufanya Ziara Ya Siku Moja Nachingwea
0
November 15, 2018
Tags