Waziri mkuu Majaliwa amsukuma ndani Mkurugenzi

Waziri mkuu Majaliwa amsukuma ndani Mkurugenzi
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemwagiza afisa usalama wa wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita, kumsaka mkaguzi wa ndani wa mahesabu ya wilaya hiyo ili akamatwe kutokana na ubadhilifu wa fedha.

Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo mapema leo, kwenye mkutano wa hadhara wilayani hapo ambapo yupo katika ziara ya kikazi, na kubainisha kuwa tayari watu 7 wameshakamatwa akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.

''Nimefika hapa, tumefanya vikao na viongozi wa halmashauri na tumebaini ubadhilifu wa fedha za miradi mbalimbali hivyo nimeagiza wahusika wote wakamatwe akiwemo mkaguzi wa ndani ambaye hajahudhuria kikao'', amesema Majaliwa.

Watumishi hao wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale akiwemo Mkurugenzi wanatuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu,  fedha ambazo zilitolewa na Serikali kwaajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo.

Mbali na hilo Waziri Mkuu amewaonya wanaume wa mkoani Geita kwa ujumla juu ya suala la kuwapa mimba wanafunzi na kusema atakayekutwa amesimama na binti katika kona isiyoeleweka atakamatwa na kwenda kutumikia adhabu ya miaka 30 jela.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad