Wizara ya Elimu Yatoa Tamko Kali Kuhusu Viboko Mashuleni

Wizara ya Elimu Yatoa Tamko Kali Kuhusu Viboko Mashuleni
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetoa tamko maalum kuhusu uchapwaji wa viboko kwa wanafunzi wanapokuwa shuleni, na kuwapa onyo walimu watakaochapa wanafunzi


Akisoma taarifa hiyo Bungeni Naibu Waziri wa Wizara hiyo William Tate OleNasha amesema kwamba kuna waraka ambao ulitolewa kisheria kwa wadau wa elimu kuhusu uchapwaji wa viboko, ambao unasema wazi utaratibu huo wa uchapwaji, na lazima iombwe kibali na kutolewa na maandishi.

“Haitakiwi vizidi viboko vinne, hairuhusiwi kwa mwalimu yeyote yule kuchapa viboko, bali ni mwalimu mkuu tu, na lazima kiombwe kibali cha kufanya hivyo, ni marufuku mwalimu yeyote kumchapa mwanafunzi kinyume na taratibu na sheria, lakini vile vile na marufuku mwalimu yoyote kutembea na viboko kwa lengo la kumchapa mwanafunzi, kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria na hatua zitachukuliwa”, alisikika Naibu Waziri wa Elimu William Tate Ole Nasha.

Hivi karibuni kulikuwa na mjadala wa kuchapwa viboko wanafunzi baada ya mwanafunzi mmoja kufariki dunia baada ya kuchapwa viboko na mwalimu wake, akimtuhumu kuiba pochi yake ambayo baadaye aliletewa na dereva boda boda baada ya kuisahau.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad