Kumekuwa na tetesi zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Lord Eyes wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini Wolper amefungukia madai hayo na kusema kuwa hayana ukweli wowote.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wolper alisema yeye ameona kwenye mitandao taarifa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Lord lakini pia hata siku ikitokea ikawa hivyo sio mbaya kwani sio mwanaume mbaya kwake na pia anavutiwa na jinsi alivyo.
Unajua hata mimi ambaye naambiwa natoka naye nimeona kwenye mitandao tu lakini pia siku ikitokea, freshi tu.Sio mwanaume mbaya maana ana sifa zote za mwanaume ninayempenda au wamesema hivyo kwa sababu niliimba wimbo wake nikauposti mtandaoni ndio tatizo basi ngoja tuone itakavyokuwa maana Wabongo wape picha tu maneno wataweka mwenyewe.”