Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu, Omar Kaya, ameeleza kuwa uongozi utaeleza kila kitu kuhusiana na uchaguzi utakaofanyika kama utakuwa ni Mkuu ama wa kujaza nafasi.
Kaya ameeleza hivyo kutokana na matamko tofauti tofauti ya klabu hiyo siku zilizopita kusema watafanya uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi ambazo zipo wazi baada ya viongozi kadhaa kujiuzulu.
Viongozi kadhaa akiwemo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, pia aliyekuwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa, waliachia ngazi na nafasi zao zikiendelea kuwa wazi mpaka sasa.
Mbali na nyadhifa hizo zilizo wazi, Yanga pia ilitoa matamko ya kueleza nafasi ya Mwenyekiti wao Yusuf Manji, itaendelea kuwepo kufuatia mkutano mkuu wa mwisho uliofanyika Juni 6 2018 kuamua Manji aendelee kukalia kiti hicho.