Kindoki alicheza mechi hiyo akichukua nafasi ya Beno Kakolanya ambaye aligoma kusaifiri kuelekea Shinyanga kwa madai ya mshahara, alifungwa bao la kusawazishwa wakati Yanga ikiwa imetangulia, bao ambalo wengi waliamini ni la kizembe.
Mashabiki hao baadhi wametoa yao ya moyoni na kueleza kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo pekee na inahitaji kipa huyo kupewa muda zaidi ili kuzoea ligi ya Tanzania namna ilivyo.
Katika mechi hiyo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo mabao yake yaliwekwa kimiani na Heritier Makambo pamoja na Mrisho Khalfan Ngassa.
Kwa sasa Yanga tayari imeshawasili mjini Kagera tayari kwa maandalizi dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Kaitaba kesho Jumapili.