Yanga Yaongeza Nguvu Yaleta Mchezaji Mmoja Kikosini

Yanga Yaongeza Nguvu Yaongeza Mchezaji Mmoja Kikosini
Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kimeandamwa na majeruhi kadhaa mpaka sasa, Uongozi wa Yanga umerejesha Mkongo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ndani ya kikosi hicho juzi Jumanne na kuanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Kiungo huyo alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo yalisababisha kukosa mechi zaidi ya tatu msimu huu kutokana na kutokuwa imara kiafya.

Mratibu wa Yanga, Hafidhi Salehe alisema kuwa mchezaji huyo ataendelea kufanya mazoezi ila mchezo wao na Reha uliopigwa jana Jumatano hakuwa ya wachezaji waliocheza kwa kuwa ndiyo kwanza ameanza mazoezi.

“Kurejea kwake ni jambo jema na la kheri kwa timu sababu anakuwa ameongeza nguvu hivyo hakuna tatizo mchezaji ambaye amesalia kwa sasa yupo nje ni Juma Mahadhi pekee,” valisema Hafidhi ambaye ni miongoni mwa watu waliodumu kwenye ofisi za Yanga zaidi ya miaka 10.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad