Zaidi ya wanafunzi 200 wa kitongoji cha Kininga B kata ya Kapalala Mkoani Songwe hawana mahali pa kusoma na kuwafanya wakose elimu kutokana
na shule waliyokuwa wakisoma kufungwa kwa kutokuwa na vigezo.
Shule ya msingi Kininga B ambayo ilianzishwa mwaka 2003 ikiwa na lengo kupunguza changamoto ya wanafunzi kusafiri umbali wa kilometa 16 kufuata
shule huku jiografia ya eneo hilo ikiwa ni milima, pia ikiwa imezungukwa na msitu wa hifadhi ambao unapitisha wanyama
Akizungumza alipotembelea shule hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Nikodemus Mwangela amesema hayupo tayari kuona nguvu za wananchi
zinapotea na kuagiza watendaji wa wilaya na mkoa
kuhakikisha wanatumia mapato yao ya ndani kujenga madarasa mawili ya mfano ndani ya mwezi mmoja, Brigedia Mwangela amesema, "Nimeyaona majengo na hayakujengwa kwenye viwango vnavyotakiwa na nimeagiza kama mkoa tutaleta mabati ya kutosha ili kujenga shule hii na wao kama wilaya wajiandae kutengeza darasa ili kunusuru wanafunzi hawa 200 pindi shule zinapofunguliwa." Amesema Nikodemus Mwangela
--