Zaidi ya Watu 23 Wafariki Kufuatia Boti Nchini Uganda Kuzama Ziwa Victoria


Watu wengine 40 wameokolewa huku boti hiyo iliyopinduka jana Novemba 24 katika Kaunti ndogo ya Mpatta Wilayani Mukono ikikadiriwa kuwa ilibeba zaidi ya watu 100

Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika hospitali ya Kampala kwa uchunguzi huku shughuli za uokoaji zikiendelea ambapo kupata Watu walio hai kwa sasa inaweza kuwa vigumu

Bado chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika lakini kubeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wake, matatizo ya kiufundi na hali mbaya ya hewa vinadhaniwa vinaweza kuwa vimechangia

Aidha, katika watu waliokolewa wapo Mwanamfalme David Wasajja, ndugu wa Mfalme wa Buganda Ronald Mutebi, Mwanamuziki Iryn Namubiru na Mfanyabiashara John Fredrick Kiyimba maarufu 'Freeman'

Hii ni ajali nyingine mbaya kutokea katika ziwa hilo kufuatia ile ya mwezi Septemba mwaka huu ambapo Kivuko kilichokuwa kimebeba watu kupita uwezo wake kilizama katika ziwa hilo nchini Tanzania na kuua zaidi ya Watu 200
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad