Tende ni matunda maarufu sana kutokana na faida kedekede zipatikanazo. Kwa kingereza huitwa dates, kwa kihindi huitwa khajur, kwa lugha ya kitaalamu (botanical name)huitwa Phoenix dactiylifera.
Tende zimetunukiwa viambata muhimu mno kama protini, wanga, vitamins B1, B3,B5,A1,pia madini kama kalsiam, magniziam, manganizi, na kopa.
Tende zinaweza kuchanganywa na maziwa ili kuongeza ufanisi, au kuchanganya na asali, unaweza kufanya juisi ya tende maridhawa, au kula hivi hivi.
Miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kutumia juisi ya tende au tende zenyewe ni kama ifuatavyo;
Kuimarisha mifupa (bones),misuli na meno, tende husaidia sana kuimarisha afya ya mifupa, misuli na meno ya mlaji. Sababu tende zina manganese kwa wingi, kalsiam, selenium, pamoja na copper.
Husaidia kuimarisha afya ya macho (eye sight), ulaji wa tende au juisi yake maridhawa. Kutokana na upatikanaji wa vitamini kwa wingi.
Husaidia kwa wenye saratani. Kama ambavyo tafiti iliyofanywa na American cancer society, ambayo inaonesha mchango wa tende katika kupambana na saratani.
Husaidia kuongeza nguvu (nishati) au energy booster).kula tende japo tatu au juisi ya tende ili kuongeza nishati katika mwili wako. Tende zina sukari ya asili kama glucose, fructose na sucrose
Hivyo humfanya mlaji kupata nishati ya kutosha na kwa haraka.
Husadia mfumo wa mmeng'enyo (digestive system). Kama unapata choo kigumu au matatizo yanayofungamana na mfumo wa mmeng'enyo jenga tabia ya kula tende japo tatu kwa siku. Tende zina dietary fibers (nyuzinyuzi )hivyo kuboresha usagaji wa chakula.
Hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo. Tende zinasaidia kwa mlaji wake kuweza kuepukana na magonjwa ya moyo, pendelea kutumia juisi ya tende.
Kuboresha afya ya ngozi yako, kuifanya iwe kwenye ubora wake. Tende zimetunukiwa vitamin B5,ambavyo huzifanya seli za ngozi zilizokufa kuwa hai.
Husaidia kuimarisha afya za wanandoa hasa wanaume, na kupunguza tatizo la udhaifu katika jimai (sexual under performance). Tende zinakiwango kikubwa cha estradiol na flavonoids ambavyo huongeza uzalishaji wa mbegu (sperms) changanya tende, maziwa na asali. Pia husaidia kuondoa tatizo la ugumba (sterility).