Zitto Kabwe kutinga Mahakamani, kisa dhamana ya Mbowe na Ester Matiko


Zitto Kabwe kutinga Mahakamani, kisa dhamana ya Mbowe na Ester Matiko
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa leo Novemba 28, 2018 atafika katika Mahakama Kuu kuonesha mshikamano, kufuatia kunyimwa dhamana kwa Kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge Esther Matiko.

Zitto amesema anaenda kuungana na viongozi  kuonyesha mshikamano dhidi ya vitendo vya kibabe, kikatili na ukandamizaji wa haki.

Wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimfutia dhamana mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, Freeman Mbowe na Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad