Zitto Kabwe Kuwasilisha Ombi la Kuachiliwa Huru Mahakamani

Zitto Kabwe Kuwasilisha Ombi la Kuachiliwa Huru Mahakamani
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe, anatarajiwa kuwasilisha ombi la kutaka kuachiliwa huru mahakamani baada yake kulala seli za polisi.

Bw Kabwe, ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini, ali kamatwana kuzuiliwa na polisi katika kituo cha polisi Oysterbay kabla ya kuhamishiwa makao makuu ya polisi kwa mahojiano zaidi. Kufikia jioni, alikuwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mburahati.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilikuwa limemtaka mwanasiasa huyo kuwasilisha vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018.

Mbunge huyo alikuwa amewaambia wanahabari kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika tukio la mapigano kati ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Alisema hilo lilitokea wakati wa kuwahamisha Wakulima katika eneo la Mpeta wilayani Uvinza mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alisema tuhuma za mbunge huyo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad