Zitto: "Tunakubali kwenda kujinyonga"

Zitto: "Tunakubali kwenda kujinyonga"
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Zitto Kabwe amesema kama wabunge hawatahitaji uwajibikaji upande wa serikali watakuwa wanapiga porojo kutokana na kutotekelezwa kwa mambo wanayokubaliana.

Akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka wa fedha 2019/20, Zitto amesema katika mpango wa mwaka 2016 walijadiliana na kukubaliana serikali ikatenge shilingi trilioni 13.2 kwa ajili ya mpango huo lakini walitoa Shilingi triloni 5 hivyo kuendelea kupitisha vitu ambavyo havifanyiwi kazi ni sawa na kukubali kujinyonga na kuendelea kuagiza bidhaa kutoka nje.

“Hii inaonyesha kama hatutakuwa makini na kuhitaji uwajibikaji upande wa serikali tutakuwa tunapiga porojo, kwa sababu kile tulichokubaliana kikafanywe wenzetu ambao tumekubaliana nao hawafanyi, Je tunakubali kwenda kujinyonga na kuwa taifa linalotegemea kuagiza mbegu kutoka nje?” amesema Zitto.

Zitto amesema serikali ina tatizo kwenye taarifa za uhasibu na kwamba ukitazama taarifa zilizopo sasa inaonyesha kuwa wanarudi katika tatizo kama la upotevu wa Shilingi trilioni 1.5 .

Zitto ameongeza kuwa katika taarifa ambazo zimetolewa na serikali za makusanyo hadi Juni, 2018 na taarifa ya fedha ambazo Serikali imezitoa kwenda kwenye mafungu kuna tofauti ya shilingi trilioni 2.1

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad