Ufafanuzi huo umetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwenda kwa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania(Tamongsco)
Katika barua hiyo iliyothibitishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Dkt. Leonard Akwilapo imezitaka shule binafsi kuwaruhusu Wanafunzi kuendelea na masomo
Dkt. Akwilapo amesema “Ni kweli tumewaandikia barua Tamongsco kwani ufafanuzi huo unatokana na maelekezo ya awali kuwachanganya na yalikuwa hayawahusu wao bali shule za umma."
Ameeleza kuwa Mwanafunzi atakayepata mimba shule ya umma ataruhusiwa kujiunga na shule ya binafsi kwa kufuata taratibu za shule husika
Aidha, Mwenyekiti Tamongsco, Mrinde Mzava amesema hajaiona barua hiyo huku Afisa Mtendaji Mkuu Shirikisho la watoaji elimu wasiotegemea Serikali kusini kwa jangwa la sahara(CIEPSSA), Benjamin Nkonya alisema ameiona