Abiria FastJet Waanza Kurudishiwa Naul Zao


Shirika la ndege la Fastjet Tanzania limeanza kuwarejeshea nauli wateja walionunua tiketi baada ya kusitisha safari zake.


Hatua hiyo imefikiwa baada ya Desemba 17, mwaka huu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuliagiza shirika hilo kuwarudishia fedha abiria wote walio kata tiketi au kuwatafutia nafasi za safari katika mashirika mengine.


Msemaji wa shirika hilo, Lucy Mbogoro, amesema baadhi ya wateja wao walianza kurudishiwa fedha hizo Jumatatu wiki hii hasa kwa wateja walionunua tiketi kwa njia ya mtandao.


“Jumatatu tulitoa tangazo kuwa tutaanza kushughulikia malipo ya wateja wetu pamoja na wadau wengine tunaofanya nao biashara, siku hiyo hiyo tulianza kushughulikia kwa wale walionunua kwa M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa.


“Ila kwa wale walionunua kwa ‘cash’ tulitangaza tutaanza kushughulikia malipo yao tarehe 20 na tayari tumeanza kulishughulikia hilo , tumekuwa tukiendelea na taratibu za benki kwa sababu hatuwezi kukaa na fedha nyingi, lazima tuzipeleke benk” amesema Lucy.


Amesema katika urejeshaji wa fedha hizo, watatoa kipaumbele kwa wateja waliotarajia kusafiri kuanzia Desemba 20, hadi 31, mwaka huu ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao, huku wale wanaotarajiwa kusafiri kuanzia Januari, wakiendelea kulipwa taratibu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad