ACT Wazalendo Yapinga Kanuni Mpya za Mafao ya Wastaafu

ACT Wazalendo Yapinga Kanuni Mpya za Mafao ya Wastaafu
Chama cha ACT Wazalendo kimepinga kanuni mpya za mafao ya wastaafu na kuitaka serikali irejeshe asiimia 50 ya mafao ya mkupuo kwa wastaafu kama ilivyokuwa awali.



Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kamimu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo,  Yeremia Kulwa Maganja amesema mnamo Desemba 1, 2018 ngome ya wazee ya chama hicho ilifanya kongamano la mashauriano ya wazee na moja ya agenda waliyoijadili ni changamoto za wazee nchini hasa wastaafu.



Katika hoja ya msingi iliyojadiliwa, amesema ilikuwa ni kuhusu kanuni mpya inayotumika kukokotoa mafao ya wastaafu ambapo amedai kanuni hiyo inamnyonya mstaafu kupata haki zake za msingi.



Maganja amesema chama cha ACT kinatoa wito kwa serikali kutumia kanuni ya awali itakayowezesha wafanyakazi kukopa mikopo ya nyumba na kuwa na uhakika wa makazi pamoja na ustawi wa maisha.



Hivi karibuni sakata la mafao limeibuka baada ya serikali kubadili kanuni ya mafao ambapo Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ilieleza sababu za kubadili kikokotoo kinachotumika kutoa mafao kwa wastaafu, ikilenga kuhakikisha kunakuwa na usawa kwa wanachama wote kunufaika na mifuko, na kusema kilichobadilika katika kikokotoo hicho kipya ni kiwango cha mkupuo kwa kundi dogo la wanachama takriban asilimia 20 ya wanachama wote wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini.



Akizungumzia kuhusu kauli ya Rais John Magufuli ambayo aliitoa jana Jumapili wilayani Arumeru akiwaomba wananchi wamuombee, ili asiye na kibri badala yake cheo cha urais kikamsaidie kuleta maendeleo chanya kwa Watanzania, Maganja amesema wao kama ACT Wazalendo Tanznia nzima hawatamuombea Rai Magufuli na akidai kuwa kufanya hivyo ni kumdhihaki Mwenyezi Mungu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad