Agizo la Mkuu wa Mkoa Laleta Taharuki Mbeya Wamachinga Wafunga Barabara

Agizo la Mkuu wa Mkoa Laleta Taharuki Mbeya Wamachinga Wafunga Barabara
 Hali ya sintofahamu imeibuka Jijini Mbeya kufuatia wafanyabiashara wa maeneo ya Mwanjelwa kudaiwa kufunga barabara kwa kile kilichoelezwa kuwa kutokubaliana na maamuzi ya Mkuu wa Mkoa huo.


Kwa mujibu Mkuu wa Mkoa wa huo Albert Chalamila aliwataka wafanyabaiashara hao kuhama kwenye maeneo ambayo yanatajwa si rasmi, na kutakiwa kuelekea kwenye maeneo ambayo yametengwa hadi kufikia siku ya ijumaa.

Kufuatia sintofahamu hiyo mapema leo disemba 3 Jijini humo Jeshi la polisi lililazimika kuingilia kati na kutuliza ghasia za wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Mwanjelwa waliokuwa wakipinga agizo la kuwataka waondoke.

Ghasia hizo za wafanyabiashara zimepelekea kufungwa kwa soko hilo baada ya kufunga barabara ya kuelekea hospitali ya Mwanjelwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad