Alichokisema Spika Ndugai Wakati wa Mapokezi ya Ndege Mpya ya Airbus 220


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema awali Tanzania ilikuwa inachekwa hadi na nchi ndogo kutokana na kukosa kitu cha kujivunia na hivi sasa wanapaswa kuunga mkono juhudi hizo na kuwa wazalendo.

Ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 23, 2018 katika mapokezi ya ndege mpya ya Airbus A220-300 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Ndege hiyo itakayokuwa inafanya kazi zake ndani na nje ya nchi yenye uwezo wa kubeba abiria 132 huku 12 kati yao wakiwa ni wa daraja la biashara.

Spika Ndugai amesema Watanzania na wafanyakazi wanapaswa sasa kutumia ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) pindi wanapofanya safari sehemu ambazo kuna vituo vya shirika hilo.

“Tuunge mkono juhudi ili kuwezesha ‘graph’ ya mauzo na mapato ya ndege zetu kuendelea kupanda kila siku na nyie bodi ya ATCL endeleeni kusimamia suala hili ili isiwe kama ile iliyopita,” amesema.

“Bodi iliyopita ilikuwa ikiangalia tu mambo, mapato yanashuka ipo tu, yanaendelea kushuka ipo tu hadi yanafika sifuri haijafanya chochote, jamani tuhakikishe hilo halitokei tena,” amesema Ndugai.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad