Alikiba amtaja msanii wa Bongo aliyemfanya ahamie kwenye muziki


Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, AliKiba amefunguka msanii aliyemfanya aingie kwenye muziki. 

Alikiba amesema kuwa amesema kuwa yeye alikuwa anapenda sana mpira lakini alivyokuwa anamuona Mr. Blue na alimwambia anataka kuwa kama yeye na msanii huyo alibali na alimwambia mpaka afike alipo yeye sio masihara. 

"Mimi nilikuwa napenda mpira nilikuwa nacheka for fun lakini Mwenyezi Mungu alinielekeza kwenye muziki nilipoenda nikafanikiwa nilikuwa nafanya fanya tu nilikuwa nawaona wakina Mr Blue wanapita pale maskani mi nilikuwa nacheza mpira," alisema AliKiba. 

"Kuna siku niliwaomba Mr Blue na Abby Skills kuwa nataka kuwa kama ninyi bwana, Mr Blue bwana alisema kama angekuwa na uwezo anifungulie niingie mzee lakini mpaka ufike hapa sio masihara lakini nilimuelewa kwasababu nilisota sana nikamwambia basi haina shida me ntakubali ntaforce kuingia akaniambia poa basi akanishika mkono tukawa pamoja na kila sehemu tukawa tunakwenda na nini lakini sikufichi mimi mpaka nakuja kutoka mimi nimetoka mwaka 2007 na hiyo story ninayokwambia ni ya mwaka 2003 ndio nakutana nao, " aliongeza Kiba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad