Amber Ruty Apigwa 'STOP' na Wchungaji Wake

Amber Ruty apigwa 'stop' na mchungaji wake
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mchungaji Daudi Mashimo wa Kanisa la Emmaus Bible Church, Mbezi Luis Dar es salaam ambaye ndiye anayewasimamia Amber Ruty na mpenzi wake jana usiku amewazuia kuzungumza na wanahabari.

Amber Ruty na mpenzi wake walifika katika moja ya hafla ya msanii wa vichekesho ili kuungana na wengine kusherehekea sikukuu ya Krismasi, ndipo mapaparazi walimsogelea na kuomba kufanya nae mahojiano juu ya maisha yake ya sasa ikiwa ni pamoja na kuonekana wakiimba wimbo wa dini na mpenzi wake.

Mchungaji: Amber naomba mrudi ndani

Mwandishi: Tunaomba kuzungumza naye mchungaji ni mambo mazuri tu.

Mchungaji: Hapana hapa tumekuja katika shughuli ya watu na lengo letu sio kuzungumza na vyombo vya habari samahani, mkiwahitaji hakuna shida watafute sehemu nyingine na wakati mwingine.

Novemba 27, 2018 Amber Rutty alidhaminiwa na ndugu yake, huku mpenzi wake akidhaminiwa na Mchungaji Daudi, juu ya kesi yao inayowakabili ya kusambaza video za ngono.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad