Anayedaiwa Kumpa Waziri Lukuvi Rushwa Akutwa na Kesi ya Kujibu


Mfanyabiashara Mohamed Kiluwa(50) amekutwa na kesi ya kujibu katika mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar na ataanza kujitetea Desemba 17 mwaka huu

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu, Samuel Obasi kufuatia upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao baada ya kupeleka masahidi 6

Kiluwa anakabiliwa na shtaka moja la kutoa rushwa ya Dola za Kimarekani 40,000 kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi

Hakimu Obasi amesema amepitia ushahidi wa mashahidi hao pamoja na vielelezo ikiwemo hati za ardhi na CD na kumuona mshtakiwa kuwa ana kesi ya kujibu.

Katika Mashahidi 6 yupo Waziri Lukuvi ambaye katika ushahidi wake alidai kuwa alipigiwa simu na msiri wake kwamba kuna fedha chafu zimepelekwa ofisini kwake
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad