Tukio hili limetokea tarehe 20/12/2018 majira ya 19:30hrs ambapo Jeshi la Polisi lilipata taarifa kuwa huko maeneo ya Mtaa wa Lumaliza kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora kijana mmoja aitwaye JUMANNE NTIMIZI, HUSSEIN, Miaka 17, Mwanafunzi kidato cha tatu katika shule ya sekondari Cheyo, alijeruhiwa na Askari anayefahamika kwa jina la E.9301 CPL ALMAS kwa kuchomwa na pasi ya umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kupigwa na kitu kizito kwenye paji la uso, mdomoni na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Chanzo cha tukio hili ni kutokana na kijana JUMANNE NTIMIZI kukutwa na bwana ALMAS akiwa amemkumbatia binti yake aitwaye AMINA ALMASI, Miaka 17, Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Cheyo karibu na nyumba yake kwa nia ya kufanya mapenzi ndipo baba mzazi wa Binti huyo alipochukua hatua ya kufanya kitendo hicho kibaya.
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP – EMMANUEL NLEY amesema Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora limechukua hatua kwa askari huyo kwani hadi sasa anashikiliwa na uchunguzi ukikamilika atachukuliwa hatua zaidi za kisheria.
Askari Polisi Amchoma Mwanafunzi Kwa Pasi ya Umeme
0
December 26, 2018
Tags