AU yaionya Burundi kutaka kumkamata Pierre Buyoya

AU yaionya Burundi kutaka kumkamata Pierre Buyoya
Muungano wa Afrika (AU) umeionya Burundi dhidi ya hatua zinazoweza kuhujumu mchakato wa amani baada ya kutolewa waraka wa kimataifa kumkamata rais wa zamani Pierre Buyoya na maafisa wengine 16.

Wanatuhumiwa kwa mauaji ya mwaka 1993 ya rais wa kwanza aliyechaguliwa nchini humo ambaye alitoka kabila la Hutu, ambapo kuuliwa kwa, Melchior Ndadaye kulisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Aidha, kuna hofu kuwa kumlenga Buyoya ambaye ni kutoka kabila la Tutsi anayeishi nchini Mali kunaweza kuchangia kuzuka misukosuko ya kikabila.

Zaidi ya watu 300,000 waliuawa kwenye vita ya miaka 12 vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi lenye watutsi walio wachache na waasi wa Hutu.

Hata hivyo, Buyoya 69, alihusika kwenye mchakato wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongoza kuchaguliwa kiongozi wa zamani wa waasi wa Hutu, Pierre Nkurunziza kuwa rais mwaka 2005.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad