Bobi Wine Azuiliwa Tena Uganda


Mbunge wa upinzani nchini Uganda na mwanamuziki wa Pop, Bobi Wine amezuiliwa kufanya matamasha nchini humo leo Desemba 26 kama alivyokuwa amepanga hapo awali.

Mapema leo katika ukurasa wake wa Twitter, Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi aliandika kuwa Polisi wametanda katika eneo la One Love Beach, wakifunga barabara zote na kutoa tangazo la kusitisha tamasha hilo.

Msemaji wa polisi nchini Uganda, Emilian Kayima amesema kwamba Bobi Wine alikuwa hajaandika barua ya kuomba ruhusa kufanya tamasha hilo ndio maana hawawezi kumruhusu.

“Tutakuwa katika ufukwe wa Busabala kuzuia shughuli hiyo na kuhakikisha usalama upo.Tamasha hili halikuwa limeruhusiwa kufanyika kwa sababu ya kutokidhi vigezo”, amesema Kayima.

Hili lingekuwa tamasha la pili la Bobi Wine kufanyika, tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad