Mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco amefunguka juu ya ndoto yake kubwa ya kucheza soka kimataifa muda wowote endapo ataipata nafasi hiyo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, yupo nchini eSwatini na klabu yake ya Simba wakipata mapumziko mafupi baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Mbabane Swallows ya nchini humo wikiendi iliyopita.
Akizungumzia kuhusu ndoto yake ya kucheza soka la kimataifa, John Bocco amesema, "bado naona nina nafasi ya kucheza soka nje ya Simba na Tanzania, ninaamini nikipata nafasi nitaitumikia vizuri".
Ikumbukwe kuwa Bocco hajawahi kucheza soka nje ya nchi, ambapo mpaka sasa amevitumikia vilabu viwili pekee vya ligi kuu Tanzania bara, ambavyo ni Azam FC na Simba SC.
Katika vilabu hivyo viwili, Bocco amefanikiwa kuweka historia ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu Tanzania bara TPL, akiwa amefunga zaidi ya mabao 100 tangu mwaka 2008 alipoanza kucheza ligi kuu akiwa na Azam FC.
Bocco ambaye yupo na kikosi cha Simba eSwatini baada ya kumaliza kazi dhidi ya Mbabane Swallows, ameeleza kuwa endapo akipata nafasi hiyo hataweza kuipoteza kirahisi.
Wakati huo kikosi cha Simba kinatarajia kuwasili leo nchini baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa ushindi wa jumla ya ma