Tanzania kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Serikali ya Watu wa China, zimedhamiria kutangaza vivutio mbalimbali nchini na kukuza biashara kati ya nchi hizo.
Akizungumza na wanahabari juzi Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo, alisema lengo kuu la ziara iliyofanyika nchini China katika Jiji la Shanghai, Guangzhou, Hong Kong, Chengdu na Beijing Novemba 12- 20, ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza utalii.
Alisema wametumia fursa hiyo kuhakikisha Tanzania inaongeza sehemu ya umiliki wa soko kwenye soko la utalii kwa kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zikizopo nchini ikiwamo na safari za ndege za ATCL kwenda China.
Jaji Mihayo, alisema katika safari hiyo ya nchini China, wameweza kusaini mkataba na Kampuni ya Touchroad Group na TTB na wamekubaliana kuwa kampuni hiyo italeta watalii 10,000 kutoka China hadi kufi kia mwaka 2019.
“Kundi la kwanza la watalii wanatarajiwa kuwasili nchini Januari na Februari 2019, watakuwa nchini kwa muda wa siku tatu na Touchroad wameonesha nia ya kuwekeza katika
huduma ya malazi zenye hadhi ya nyota tano na tayari wanazo hoteli nne,” alisema Jaji Mihayo.
Katika ziara waliyoifanya ya Jiji la Beijing, wawakilishi wa Shirika la Utangazaji la China (CCTV), walikutana na maofisa wa MNRT na wakatoa mapendekezo ya kutengeneza makala za dakika 30 za zamadam kisha kutoa filamu kama
ya Jurassic Park, ili kurushwa kwenye televisheni yao.
“Pia, CCTV4 wameafiki kushirikiana na Wakala wa Misitu
Tanzania (TFS), kupiga picha katika hifadhi za asili za misitu wakati wa sherehe za maadhimisho ya mwaka mpya wa China mnamo mwezi Februari 2019,” alisema.
Mwenyekiti huyo wa TTB alisema kwa takwimu inaonesha Tanzania kwa mwaka 2017 imeweza kupokea watalii 29,224 kutoka nchini China wakitembelea vivutio tofauti nchini.
Kwa upande wake, Meneja Mauzo na Usambazaji wa ATCL,
Edward Nkwabi, alisema katika ziara hiyo walipokea maombi kutokakwa viongozi wa miji ya Hong Kong, Beijig, Chengdu na Shanghai, kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi kwenye miji hiyo.
Alisema jambo hilo liliwafanya kuingia makubaliano na kampuni moja ya uwakala ambayo itatangaza na kuuza tiketi za safari za ndege za ATCL.
Alisema safari za moja kwa moja kuelekea nchini China zitaanza mapema mwakani kwa ajili ya kuimarisha sekta ya utalii nchini na lengo kuu ni kuwapa fursa ya kuja moja kwa moja kutoka China hadi Tanzania.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), China Kutangaza Vivutio vya Utalii Nchini
0
December 26, 2018
Tags