Wanafunzi wawili wafariki na wengine 6 wajeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu la kurushwa kwa mkono Amhara nchini Ethiopia.
Wanafunzi wawili wafariki na wengine 6 wajeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu la kurushwa kwa mkono Amhara nchini Ethiopia eneo la Gondar. Tukio hilo limefahamishwa kutokea baada ya wanafunzi hao kuchezea bomu hilo bila ya kufahamu ni kipi kinaweza kutokea.
Wanafunzi wawili wamefariki katika eneo la tukio na wengine sita wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu.
Enyewe Zewdie, msemaji wa jeshi la Polisi Amhara amewaambia waandishi wa habari kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kutambua ni vipi bomu hilo la kurushwa kwa kutumia mikono lilikuwa karibu na eneo la shule ambapo kunapatikana watoto.