Muigizaji wa filamu Natasha, ambaye pia ni mama mzazi wa msanii Monalisa, amesema anamshukuru Mungu kwenye Bongo Movie, wasichana sasa hawavai nguo fupi na zisizo na maadili kama zamani badala yake kiki na mambo hayo yamehamia kwenye Bongofleva.
gizaji Natasha
Akiongea na eNewz ya East Africa Television, Natasha amesema ''Baada ya Baraza la sanaa kusimamia vizuri na kuchukulia hatua wasanii waliokuwa wakitumia kiki mpaka kuvua nguo kwa sasa wasanii hao wametoweka na wamehamia kwenye muziki kitu ambacho kwa sisi Bongo Movie tunajivunia''.
Pia nguli huyo amefunguka kwamba kwa upande wake anaona kwa mwaka 2018 kazi za filamu Tanzania zimelipa sana tofauti na miaka ya nyuma.
Natasha anasema mwaka huu makampuni binafsi yamejitokeza kwa wingi kw aajili ya kununua filamu na kuzisambaza tofauti na zamani kampuni ya kununua filamu ilikuwa ni moja na kununua filamu yako ni mpaka umpigie magoti ndo anunue.
"Kwa kweli mimi nimekuwepo tangu miaka ya makundi ya Kaole mpaka sasa na kwa mwaka huu naweza nikasema huu mwaka umekuwa na neema na baraka kwa waigizaji kwani umeleta mafanikio mengi ikiwemo ongezeko la wanunuzi wa mtandaoni kitu ambacho kimeinua soko la filamu'', amesema.