
Bulaya amesema hayo leo Desemba 4, 2018 wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu kikokotoo hicho na kusema kupongezwa na Spika Job Ndugai kuhusu asilimia 25% ya mafao ya wastaafu hakuondoi ukweli kuwa chanzo ni wabunge wa CCM kutumia uwingi wao na kukataa mawazo ya mbadala ya kambi ya upinzani.
“Tunamtaka Waziri husika (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Walemavu) atoke na aseme ni kwanini mchakato huu wa kubadili kikokotoo haukupita kwenye vikao halali kabla ya kufika hapo. Mimi kama Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu na jopo langu, tutahakikisha tunaandaa muswada binafsi na kuupeleka Bunge kama tu kikokotoo hiki hakitarekebishwa,” amesema Bulaya.