CAF limeipokonya uenyeji wa AFCON 2019 taifa la Cameroon

CAF limeipokonya uenyeji wa AFCON 2019 taifa la Cameroon
Shirikisho la soka Afrika CAF baada ya kikao cha kamati ya utendaji cha shirikisho hilo kukutana nchini Ghana katika jiji la Accra, wamekubaliana kwa pamoja kuipokonya wenyeji wa fainali za mataifa ya Afrika nchi ya Cameroon zilizopangwa kuchezwa mwakani 2019.
CAF wametangaza kuipokonya uenyeji Cameroon na kutangaza taifa linalotaka kuwa mwenyeji litume maombi ndani ya mwezi kutokea sasa, kabla ya shirikisho hilo kufunga zoezi hilo na kufanya uamuzi baada ya kupitia maombi ya mataifa hayo licha ya Morocco kuwa inaweza kupewa uenyeji.

Uamuzi huo wa CAF unakuja ikiwa zimepita siku chache toka shikisho hilo  litume wajumbe wake nchini Cameroon kwenda kukagua mambo mbalimbali, hivyo inatajwa inawezekana miundombinu au hali ya usalama ndio imepelekea kufikia maamuzi hayo japo haijatajwa sababu rasmi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad