Calisah Aanika Mastaa Aliobanjuka Nao


Mwanamitindo maarufu wa kiume Bongo ambaye pia hivi sasa ni Mr. Africa Calisah Abdul ameanika Listi nzima ya mastaa wa kike ambao amewahi kuwa nao kwenye mahusiano.

Calisah amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Kipindi cha Ala Za Roho ya Clouds Fm ambapo alimsanua Diva The Bawse kuwa ameshakuwa kwenye mahusiano wasanii Kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, na Jacqueline Wolper.

Calisah ameweka wazi kuwa alianza mahusiano ya kimapenzi na Wema wakati bado akiwa kwenye mahusiano na Idris Sultan bila Idris mwenyewe kujua.

Lakini pia Calisah ameweka wazi kuwa ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wasanii wa Bongo movie Kama vile Irene Uwoya na Staa mwingine Jacqueline Wolper.

Kwenye mahojiano hayo Calisah amekana  kuwa kwenye mahusiano na Hamisa Mobetto na Socialite maarufu kutoka Kenya Vera Sidika na kukiri iliyotrend kwenye mitandao ni Kiki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad