Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amemtaka mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kujibu maswali kuhusu mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.
Kulingana na kituo cha habari CBC, Justin Trudeau ameyazungumza hayo katika mkutano wa G20 uliofanyika nchini Argentina.
Justin Trudeau amezungumza na Mohammed bin Salman katika mkutano huo na kumtaka ajibu maswali ambayo mpaka hivi sasa ni kitendawili kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia aliyekuwa akifanya kazi katika gazeti la "The Washington Post" nchini Marekani.
Kulingana na ripoti ya CIA ya Marekani,mauaji ya Jamal Khashoggi yaliamrishwa na mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman mnamo 2 Oktoba 2018.
Licha ya serikali ya Saudi Arabia kuikanusha ripoti hiyo,viongozi wengi wamekuwa wakimtaka Bin Saklman aeleze kwa kina kuhusu mauaji hayo.
Viongozi wengi waliohudhuria mkutano wa G20,wametumia fursa hiyo kujaribu kutatua kitendawili cha ni nani aliyehusika na kuuawa kwa Jamal Khashoggi.
Khashoggi aliuawa wakati alipoingia katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Aliingia katika ubalozi huo kufuatilia makaratasi yake kwa ajili ya kufunga ndoa.