CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015/20, ikiwa ni katika kutoa huduma bora kwa wananchi likiwemo kundi la watu wenye mahitaji maalumu.
Hayoyalisemwa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM (NEC), Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuph Nassor , wakati akikabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali katika kituo cha kulelea watu wenye mahitaji maalumu cha Cha Mission of Charity , Mburahati, Wilayani Ubungo,
Kituo hicho kina lea watu wenye mahitaji maalimu zaidi ya 100 wakiwemo, watoto waliotupwa au kutelekezwa baada ya kuzaliwa, wenye ulemavu, wazee na masikini.
“Dhamira ya CCM ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu. Lakini pia kusaidia watu wenye mahitaji maalumu. Chama kimeamua kutoa msaada wa chakula, sabuni na mahitaji mengine katika kituo hiki,”alisema Nassor.
Alitoa wito kwa wadau wengine hususan serikali kuendelea kuhudumia kituo hicho ambacho kina mahitaji mengi.
Sambamba nahilo mjumbe huyo wa NEC, aliitaka jumuiya za wazazi , UWT,na vijana, kusimamia kikamilifu suala la maadili katikajamii.
“Jumuia hizi za Chama ndiyo zinajukumu kubwa la kusimamia suala zima la maadili katika jamii ambayo hivi karibuni yamekuwa yanayumbayumba,’alisema.
Akipokea msaada huo Kiongozi wa Huduma wa Kituo cha Mission of Charity Sista Lily Thomas, aliishukuru CCM hususan kata ya Mburahati kwa misaada hiyo.
Naye Sister Maria Joseph, alisema, miongoni mwa changamoto kubwa inayo kikabili kituo ni ubovu wa barabara inayo ingia kituo hapo pamoja na miundombinu ya kupitishia maji machafu ambayo wakati wa kiangazi inaziba na kutapisha maji hayo katika kitu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM kata ya Mburahati, John Exavery Mapunda alisema, Chama kitaendelea kusaidia kuwa karibu na kituo hicho ili kusaidia mahitaji mbalimbali ya msingi.
“Mbali na hilo, alisema Chama kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kinaibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani,”alisema Mapunda..
Pamoja na hayo, Jumuia ya Wazazi Kata ya Mburahati iliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2018 mbele ya kikao cha Bara la Wazazi, na Wanachama na kumpongeza Mwenyekiti Rais Dk. John Magufuli kwa kasi kubwa ya utekelezaji wa ilani.