CCM yanyoosha Mikono kwa Jenista Mhagama

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Ndg. Humphrey Polepole kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani wa Ruvuma, Jenista Mhagama kwa kuekeleza kwa asilimia kubwa Ilani ya chama hicho.


Kushoto ni Rais Magufuli akimkabidhi Jenista Mhagama Ilani ya CCM wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015.

Polepole ametoa pongezi hizo jana jioni katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Peramiho, ambapo aliweka wazi kuwa jimbo la Jenista limekuwa mfano kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 - 2020.

"Mwenye sifa apewe, ili kuendelea kumpatia moyo wa kutenda zaidi, Ndg. Jenista Mhagama amefanya vizuri sana katika kuchochea maendeleo ya hapa Jimboni, ni mfano bora kwa wabunge wetu wa CCM" alisema Ndg. Polepole.

Pongezi hizo zilitokana na taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo ambapo kila kiongozi wa CCM wa Kata alieleza maendeleo na miradi ya wananchi  katika eneo lake iliyotekelezwa kwa ufasaha.

Mbali na pongezi hizo Polepole pia alikabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo pikipiki 16 kwa makatibu wa CCM wa Kata zote za Jimbo la Peramiho, Baiskeli 132 kwa makatibu wa CCM wa  matawi yote ya Jimbo la Peramiho, mabati 835 na Mifuko  1230 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM Jimbo la Peramiho.

Mkutano huo Mkuu wa Jimbo ulihudhuriwa na Wajumbe wa Kikao hicho, Viongozi wa Chama, Wilaya na Mkoa pamoja na Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndg. Oddo Killian.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad