CHADEMA Yatawanya Wabunge Wake

CHADEMA yatawanya wabunge wake
Vumbi la uchaguzi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limeanza kutimka katika maeneo mbalimbali ya nchi huku kikiwa kimepanga safu ya viongozi kwenye maeneo hayo kwaajili ya kusimamia chaguzi.

Uchaguzi huo unahusisha viongozi wa matawi, Kata, majimbo, mikoa na ngazi ya Kitaifa ulianza mapema mwezi huu ambapo wabunge wa Chadema wamegawana maeneo mbalimbali ya kusimamia.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema John Mrema amesema kuwa, uchaguzi huo unaenda sambamba na vikao vya ndani kwaajili ya wagombea kupata nafasi ya kujinadi.

Amesema kutokana na kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara nchini uchaguzi huo unatumia vikao vya ndani ambavyo hatahivyo katika baadhi ya maeneo vimekuwa kaa la moto huku chama kikiwatumia viongozi wenye ushawishi mkubwa wakiwemo wabunge kuongoza zoezi hilo.

"Huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya Chama na ndio maana tuko nchi nzima, tumesambaa kwa ajili ya kusimamia ili tuweze kuapata viongozi wazuri kuanzia ngazi ya msingi", amesema Mrema.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ameshika majimbo ya Momba, Tunduma, Vwawa, Mbeya Mjini na Vijijini wakati Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akisimamia majimbo yote ya mkoa wa Rukwa.

Mbunge wa Mbeya mjini, Jospeh Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ anasimamia jimbo la Njombe Mjini.

Desemba 16, 2018 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA -Zanzibar, Salum Mwalimu alikamatwa na Jeshi la Poilisi akiwa mjini Mafinga mkoani Iringa alikokwenda kushiriki moja ya kikao cha ndani akitokea Kanda ya Nyasa, ambapo kiongozi huyo ni moja ya safu iliyopangwa kusimamia chaguzi hizo katika majimbo ya Makambako, Makete, Ismani na Iringa Mjini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad