Chama Amkabidhi Jezi Shabiki Aliyemuahidi Kumpa Mke Wake

Chama Amkabidhi Jezi Shabiki Aliyemuahidi Kumpa Mke Wake
Kiungo wa Simba, Claytous Chama amemkabidhi jezi maalumu shabiki wake ambaye aliingia na bango maalumu uwanja wa Taifa likiwa limeandikwa kwa Lugha ya kiingereza kumtaka kiungo huyo ampe jezi namba 27.

"Chama 27 kama utanipa jezi yako, basi mimi nitakupatia mke wangu," lilisomeka hivyo bango lake na baada ya Chama kuliona bango hilo hakusita kumjibu kupitia ukurasa wake wa Istagram ambapo aliwaomba marafiki na jamaa wamtafute shabiki huyo.

"Namtafuta huyu jamaa, kuna jezi yake maalumu nimemuandalia ingawa sitamchukua mke wake, nisaidieni kumtafuta huyu shabiki ili niweze kutimiza ndoto ya kumpatia jezi," alisema.




Hatimaye leo amefanikiwa kumpata shabiki huyo na kumkabidhi jezi yenye namba 27 na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho watakapocheza na Nkana FC kujaza uwanja wa Taifa.

"Leo mapema nimepata bahati ya kuonana na shabiki yangu rafiki yangu Mtakatifu Mnyama ambaye aliomba jezi yangu nimefanikiwa kutimiza ndoto yake," alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad