Coke Studio Afrika Imewaleta Wasanii wa Muziki Toka Maeneo Mbali Mbali ya Bara la Afrika Msimu Mpya Utakao Oneshwa Kwenye Television Mwaka 2019
0
December 11, 2018
Kufuatia mafanikio makubwa ya uzinduzi na utayarishaji kwa msimu wa Coke Studio
Africa wa mwaka 2019 jijini Nairobi – Kenya, Kampuni ya Coca-Cola imeyaweka wazi
majina zaidi ya 25 ya wasanii wenye vipaji toka barani Afrika ambao watashiriki kwenye
msimu mpya ujao wa ‘Coke Studio Africa 2019’. Wasanii na watayarishaji wa muziki
kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Nigeria na
nchi zingine kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika ambao watakuburudisha
kwa mwaka ujao, kuanzia mwezi Februari 2019, ambapo kipindi kitakapo anza kuruka
kwenye kioo cha televisheni yako kote barani Afrika. Kwa mara nyingine tena, wapenzi
wa kipindi watapata kushuhudia msisimko wa mchanganyiko wa muziki, marudio ya
nyimbo za zamani, na utengenezwaji wa nyimbo mpya.
Kama wimbo wa “Vimbada” toka kwa nyota wa muziki nchini Kenya Moji Short Baba
atapata nafasi ya kushiriki Coke Studio Africa kwa mara ya kwanza akiwa na Naiboi,
kwa sasa anatamba na kibao chake cha “2 In 1”, Nguli wa muziki wa kufoka foka (Hip-
Hop) Khaligraph Jones, ambaye hivi karibuni ametwaa tuzo ya kuwa mwana muziki bora
wa Hip-hop barani Afrika mwaka 2018 katika tuzo za AFRIMMA, atarudi kwa mara ya
pili katika msimu huu mpya. Kutoka Tanzania msanii nyota wa bongo flava na mshindi
wa tuzo ya BET Rayvanny pamoja na mwanadada mwenye sauti nyororo ‘Nandy’
wataungana na kubariki kipindi kwa mara ya pili.
Baadhi ya washiriki wapya wenye msisimuko kwenye kipindi ni Harmonize ambaye
alitamba na kibao chake “Kwangaru” na Juma Jux, mkali wa muziki wa R&B na msanii
kutoka Mdee Music, Mimi Mars. Uganda watawakilishwa na mshindi wa tuzo nyingi
mwanadada Sheebah, akirudi kwenye msimu kwa mara ya pili. Ataungana na wasanii
maarufu mbali mbali wa nchini Ethiopia akiwemo Mahelt, na wenyeji kama Bisrat,
Abush Zekele, Yared Negu na Rophnan Nuri.
Ladha ya burudani toka Magharibi mwa Afrika italetwa na watayarishaji wakali wa
muziki, GospelOnDeBeatz na nyota wa muziki nchini Nigeria Skales na RudeBoy
(alikuwa akiunda kundi la P Square) watakavyo ling`arisha jukwaa kwa utumbuizaji wa
hali ya juu na vibao matata. Utayarishaji wa Coke Studio Africa 2019 unaendelea, kwa
nyimbo za kushirikiana za wasanii na waandaaji wa muziki watakao tengeneza muziki
utakao waunganisha watu kutoka barani Afrika. Itahusisha zaidi ya nyimbo halisi 10
zilizotengenezwa na mtiririko wa kipekee kwa msimu chrisimass kwa mwezi huu wa Dec
2018 kutoka coke studio Afrika. Msimu huu unao subiriwa kwa hamu utakuwa
ukiadhimisha aina mbali mbali za muziki na tamaduni. Itakuja pamoja na kuwa chanzo
cha kusheherekea maudhui ya kiafrika na muziki, kutanabaisha hadithi na muunganiko
ambao hupaswi kuukosa.
MAONI YA MHARIRI
Coke Studio Africa ni shoo isiyo ya mashindano ya muziki, ambayo inataka kuleta
pamoja, na kusheherekea utofauti wa muziki wa Afrika na vipaji. Na pia inawapa nafasi
wasanii wanaochipukia kufanya kazi na baadhi ya wakali wenye vipaji toka ndani na
kimataifa. Wasanii wanatolewa toka kwenye aina mbali mbali za muziki, muda na
maeneo tofauti na kuwekwa kwenye jozi (kuoanishwa) ili kutengeneza muziki wa kisasa
na halisi wenye sauti nzuri za Kiafrika kupitia mchanganyiko wa muziki. Jinsi wasanii
watakavyo husiana na kutengeneza muziki utakao wekwa kwenye kumbukumbu na
watayarishaji. Pia watapata nafasi ya kujifunza kuhusu muziki wa kila mmoja na mitindo
wakati wakibadilishana tamaduni. Shoo inampeleka mtazamaji ndani ya studio ya
kurekodi na kutazama mchanganyiko wa wasanii mbali mbali.
Washirika rasmi wa coke studio Africa 2019 ni; Sankara Hotel, PACE Africa, Yallo na
Home 254. Pamoja na Pace Africa, wasanii watapata kufurahia ubora wa muziki wa hali
ya juu kupitia Vifaa vya sauti za masikio (headphones) zenye chapa ya Coke Studio
vitakavyo tolewa na kampuni ya Pace. Aina nyingine ambayo itakuwa na chapa ya Coke
Studio ni mavazi yenye chapa (Coke Studio) ambayo yatatangenezwa na kampuni ya
mitindo: Home 254 na Yallo, ambao wanatengeneza bidhaa imara kama, Mabegi ya
ngozi. Sankara hoteli itatoa huduma bora ya malazi kwa nyota wa Coke Studio Africa
kwa muda ambao watautumia wakiwa katika studio za kurekodi kwenye coke studio
Africa jijini Nairobi, Kenya.
- kama unahitaji taarifa zaidi tafadhari wasiliana nasi kupitia press@anyiko-pr.com
-tafadhari unaweza kupatapicha za wasanii wasiliana nasikwa simu +254721368983
KWA MENGI:
YouTube: www.youtube.com/cokestudioAfrica
Facebook: www.facebook.com/cocacola
Blog: www.cokestudioafrica.com
Instagram: @CokeStudioAfrica
Twitter: @CocaColaAfrica
Hashtag: #CokeStudioAfrica
Tags