Karibu data za watu 1000 waliohama Korea Kaskazini zimevuja baada ya kompiuta huko Korea Kusini kudukuliwa, kwa mujibu wa Korea Kusini.
Kompyuta binafsi kwenye kituo cha serikali iligunduliwa kuathiriwa na kirusi.
Wizara ya mapatano nchini Korea Kusini ilisema huu unachukuliwa kuwa uvujaji mkubwa wa taarifa za wale waliohama Korea Kaskazini.
Wadukuzi na mahala udukuzi wenyewe ulitokea haijathibitishwa.
Familia za waliohama Korea Kaskazini ziko hatarini?
Serikali ya Korea Kaskazini bado haijatambua raia wote waliohama nchi hiyo. Wengine wanaweza kutajwa kuwa watu waliopotea au wamesajiliwa kuwa watu waliokufa.
Raia 997 waliohama Korea Kaskazini kwa sasa wamejulishwa kuwa majina yao, tarehe za kuzaliwa na anwani zao zimevuja lakini bado athari zake hazijulikani.
Idadi ya wanaohama Korea Kaskazini wakienda Korea Kusini yapungua
Wadadisi wanasema kuwa kuna wasi wasi kuwa kuvuja huku kunaweza kuhatarisha familia za wale waliohama ambazo bado zimebaki Korea Kaskazini.
Sokeel Park anasema udukuzi huu utasababisha watu wengine waliohama wanaoishi nchini Korea Kusini kuhisi kukosa usalama na kuchangia wao kubadilisha majina yao, namba za simu na anwani zao.
Korea Kaskazini imehusika kwa udukuzi wa awali?
Wataalamu wa usalama wa mitandao wamekuwa wakionya kuhusu kuendela kuboreka kwa mbinu zinazotumiwa na wadukuzi kutoka Korea Kaskazini.
Mwezi Septemba waendesha mashtaka nchini Marekani walimfungulia mashtaka mwanamume raia wa Korea Kaskazini ambaye amekuwa akihusika na kuunda kirusi kilichovuruga mifumo ya afya ya Uingereza.
'Kifaa' cha Korea Kaskazini chashambuliwa na K. Kusini
Moja ya udukuzi mkubwa zaidi uliohusishwa na Korea Kaskazini miaka ya hivi karibuni ulilenga kampuni ya Sony mwaka 2014.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini mara kwa mara vimetishia kuwazima wale waliohama nchi hiyo walio nchini Korea Kusini ambao huushambulia kwa maneno utawala wa Korea Kaskazini.
Data za watu 1000 waliohama Korea Kaskazini zavuja kufuatia udukuzi mkubwa nchini Korea Kusini
0
December 28, 2018
Tags