DC Katambi Awapa Onyo Wabunge wa Upinzani Wanapokuwa Bungeni

DC Katambi Awapa Onyo Wabunge wa Upinzani Wanapokuwa Bungeni
Wabunge wanaotoka Vyama vya Upinzani nchini wametakiwa kufuata sheria na taratibu pindi wanapoenda kwenye vikao vya Bunge Jijini Dodoma, na wala wasifanye shughuli ambazo zitapelekea kutiwa nguvuni na vyombo vya dola.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobasi Katambi .

Katambi amebainisha kuwa hajawahi kukutana na wabunge wa upinzani pindi wanapokuja kwenye vikao vya bunge Jijini Dodoma, lakini amewaahidi atawashughulikia endapo watafanya makosa ambayo wamekuwa wakifanya sehemu nyingine.

"Mimi sijawahi kukutana na mbunge yeyote wa upinzani lakini kila wanapokuja Dodoma lazima wafuate sheria, na taratibu za nchi kwa sababu Dodoma ni makao makuu ya nchi, serikali na chama kinachoongoza dola kwa hiyo wanapokuwa hapa wafanye kazi za kibunge na si vitu vingine kwa sababu watakuwa chini yangu kama Mkuu wa wilaya." Amesema Katambi.

Akijibu swali juu ya kauli hiyo kama hadhani inalenga kuwatisha wabunge wa upinzani Katambi amesema;  "Siwatishi na wala simtishi mtu yeyote awe mbunge au mtanzania yeyote waje tu lakini lazima akifika Dodoma afuate sheria, na aoneshe uzalendo anapokuwa Dodoma."

Mapema wiki hii Mkuu huyo wa Wilaya aliweka masharti ya kuelewana na Mwenyekiti wake wa zamani Freeman Mbowe kuwa lazima ajipambanue kuwa ni mtu ambaye anaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali.

Katambi pia alikanusha madai ya kufanya udhalilishaji kwa baadhi ya watuhumiwa ambao amekuwa akiwakamata na kuwaonesha kwenye vyombo vya habari.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tena hapo Keko gesti na Chako NI Chako ukikuta unasweka ndani bila huruma...

    HONGERA SANA DC WANGU.. JIJI LETU NI LA HESHIMA NA LAZIMA LIHESHIMIKE.
    HATA WASIO JIHESHIMU NI LAZIMA WALIHESHIMU..

    DODOMA YETU INASTAHA ZAKE NA LINI LAZIMA ISTAHIKE KAMA ILIVYO NA USTAARABU NA HESHIMA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad