Dhamana ya Mbowe, Matiko Bado Kitendawili

Dhamana ya Mbowe, Matiko Bado Kitendawili
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), bado anasubiri mwenendo wa uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, uliotupilia mbali pingamizi lake la awali dhidi ya rufani ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, wanaoendelea kusota mahabusu.

Novemba 30, mwaka huu Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ilisikiliza pingamizi la awali la DPP la kutaka rufani ya kupinga kutenguliwa dhamana ya walalamikaji Mbowe na Matiko isisikilizwe, itupiliwe mbali.

Hata hivyo, walalamikaji kupitia mawakili wao, Peter Kibatala, Jeremia Mtobesya na Dk. Rugemeleza Nshala, waliiomba mahakama kutupilia mbali pingamizi hilo.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Sam Rumanyika, ilikubaliana na hoja za walalamikaji kwa kutupilia mbali pingamizi la mlalamikiwa DPP, kwamba halina mashiko kisheria.

Mlalamikiwa hakuridhika na uamuzi huo aliwasilisha kusudio Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Jaji Rumanyika.

Jaji Rumanyika alisitisha mwenendo wa kesi hiyo hadi Mahakama ya Rufani itakaposikiliza na kutoa uamuzi wa rufani ya DPP.

Mbowe na Matiko wamekata rufani Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa kuwafutia dhamana kwa sababu waliidharau na kukiuka masharti ya dhamana ya mahakama hiyo.

Walifutiwa dhamana kwa madai kwamba hawakufika mahakamani kuhudhuria kesi inayowakabili ya uchochezi, Novemba Mosi na 8, mwaka huu na taarifa za kutokuwapo zilikinzana.

Mbowe na Matiko walipelekwa mahabusu na kesi ya msingi itatajwa Desemba 6, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad