Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameibuka na kutia neno Baada ya video iliyomuonyesha Naibu Spika Dr. Tulia Akson akiwa anacheza na kuimba wimbo wa ‘Mwanza’ uliofungiwa.
Mwezi uliopita Baraza la Sanaa Tanzania liliufungi rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ ulioimbwa na Diamond Platnumz kushirikiana na Rayvanny kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania.
Siku chache zilizopita video iliyowaonyesha viongozi mbali mbali wa Bunge ikiwemo Dr. Tulia wakicheza wimbo wa Mwanza wakiwa anasheherekea ushindi wake dhidi ya Uganda ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ametoa neno kuhusu video hiyo huku akimshukuru sana kwa sapoti:
Alichoandika Kupitia Instagram
Nimepata taarifa kuwa kwenye Mechi ya soka dhidi ya Uganda , Viongozi wetu, wameshinda…Ushindi wao ni Ushindi wetu sote…..Nawapongeza sana na shukran pia kwa Sapoti yenu kubwa juu ya kazi zetu.. japo natamani siku moja Mashabiki zetu pia wapate walau uhuru wa kuimba na kufurahia nasi Wimbo huu pendwa, kama hivyo….. #MWANZA #NYEGEZI