Diamond na Rayvany Waichezea Basata Masharubu..Waimba Wimbo wa Nyegezi Uliofungiwa Mwanza

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) linefungukia kitendo cha Wasanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Rayvanny kuperfom wimbo wao wa Mwanza ambao umefungiwa.

Mwezi uliopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuufungia rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ kwa madai kuwa wasanii hao wamekiuka maadili ya Kitanzania kwa maudhui ya wimbo huo.

Diamond aliimba wimbo huo alioshirikishwa na Rayvanny jana Desemba 15, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza jana, huku maelfu ya mashabiki wakimshangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba. Mkali huyo wa Bongo Fleva aliimba wimbo huo  akiwa pamoja na Rayvanny.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Katibu mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza alifungukia ishu hiyo na kusema:

Nimepigiwa simu kuhusu hii kitu. Niko Arusha kikazi nimeshawasiliana na mwenyekiti wa bodi (ya Basata).
Basata itakuja na majibu muafaka kwani hapa (Diamond) kaonyesha kiwango cha juu cha dharau kwa baraza, bodi, wizara (Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo) na Serikali kwa ujumla”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad