Diamond na Team yake ya Wasafi Waibukia Kenya Kufanya Show....Waelekeza Kilichotokea Kati yao na Basata


Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz amefafanua kilichotokea kati yao na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) hadi wakaruhusiwa kuondoka nchini humo kwenda Kenya kutumbuiza.

Diamond, akiandamana na mwenzake Rayvanny, amewaambia wanahabari kwamba waliiandikia serikali barua kueleza kwamba walikubali walikuwa wamekosea kuucheza wimbo wa Mwanza uliofungiwa kwenye shoo yao eneo la Mwanza mwishoni mwa wiki.

Walijitetea kwamba awali, hawakuwa wameucheza wimbo huo kwenye shoo zao.
Kadhalika, walieleza kwamba marufuku dhidi yao ingewaharibia sifa na pia kuwasababishia hasara kutokana na tamasha zao walizokuwa wameandaa kipindi hiki cha sikukuu.

“Na tukawaambia pia kwamba tuna shoo nyingine ambazo ziko Kenya, na sehemu tofauti ambazo tayari zishalipwa (tiketi zishalipiwa),” amesema Diamond.
“Kwa hivyo, tusipotumbuiza pia tutatengeneza picha mbaya, pia na hasara kwa sababu pia sisi tunafanya biashara.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad