Diwani wa Zamani Ajinyonga Hadi Kufa Kwa Kutumia Mtandao


Asha Ali Abei(55), Diwani wa zamani Kata ya Nyerere amejinyonga usiku wa kuamkia leo Desemba 26 huko shehia ya Magomeni, mkoani Mjini Magharibi, Zanzibar

Kaimu Kamanda wa Polisi, Kheri Musa amesema alifunga mtandio huo dirishani na kujinyonga, majirani walipata taarifa baada ya mtoto wa marehemu kupiga kelele, asubuhi

Jirani mmoja amesema huenda alijinyonga kutokana na msongo wa mawazo kwa madai kuwa wiki iliyopita alionekana kutokuwa na raha akidai huenda alikuwa akikabiliwa na madeni mengi

Sheha wa shehia ya Magomeni, Rajab Ali Ngauchwa amesema si vema Wananchi kuchukua hatua za haraka katika mambo yanayowachanganya ni vizuri familia kukutana na kujadili ili kupata ufumbuzi wa tatizo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad