Dkt. Angeline Mabula amuokoa mama aliyesoma naye


 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi pia Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dk. Angeline Mabula amemnusuru Mama mmoja aliyesoma naye Shule moja  anayejulikana kwa jina la Sabina Simba Mkazi wa Mecco kwa wananchi waliokuwa wakimtishia maisha  kwa kumuhusisha na imani za kishirikina. 

Mheshimiwa Daktari Mabula wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya  Mecco na Nyasaka zilizopo katika  Wilaya ya Ilemela ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza kero, changamoto na ushauri kutoka kwa wananchi wa jimbo lake, aliwataka wakazi wa eneo hilo kuachana na imani potofu juu ya mama huyo kwani anamfahamu vizuri tabia toka wanasoma. 


Mabula ametumia  fursa hiyo kuwasisitiza juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali itikadi kwa maendeleo ya Taifa, ambapo amemtaka Mwenyekiti wa eneo hilo kusimamia haki na kushughulikia mara moja suala linalomkabili mama huyo ikiwemo kukamatwa kwa watu wanaonyanyapaa. 

"Katika Kata hii kuna itikadi za vyama ukienda mtu ambaye ni chama tofauti na uongozi wa mtaa unacheleweshewa kupewa huduma muda mwingine wanakupuuzia, kama kilio cha mama Sabina huyu mama anafanyakazi Bugando hana ubaya na watu lakini alipoenda kupeleka malalamiko hayo kwa mwenyekiti juu ya kunyanyasika na kutishiwa maisha hakupewa ushirikiano wowote, hata kwenye miradi wanakuwa wanabagua miradi wamekuwa wanabagua, alisema Mabula. 

Naye Diwani wa Kata ya Mecco Godlisten Kisanga alimshukuru Mbunge kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha wananchi wa wananufaika na miradi ya maendeleo inayotolewa na Taasisi ya Angeline Foundation kwa kushirikiana na halmashuri ya manispaa ya Ilemela. 




Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nundu Kata ya Mecco, Emmanuel Kahabi alimuhaidi Mheshimiwa Mbunge kuhakikisha anamaliza tofauti kati ya Mama Sabina na wakazi wa eneo hilo kwani na kukiri malalamiko hayo kutishiwa maisha  aliyapokea muda mrefu, ambapo amemuomba Mbunge asichoke pale waendapo kuomba msaada kwani watampa ushirikiano kama hapo awali. 

Aidha, awali Mama Sabrina Simba alimpelekea malalamiko na kutaka kuomba msaada kwa Mheshimiwa Dk. Mbunge Angeline Mabula  ya kunyanyaswa na baadhi ya wakazi wa Kata yake ya Mecco wakimtaka ahame sehemu anapoishi ikiwemo kumtishia uhai kutokana tabia za kishirikina anazohusishwa kuzifanya yeye na familia yake. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad